22 Septemba 2025 - 19:19
Malta Yaitambua Rasmi Palestina

Malta imetangaza kuwa leo itaikubali rasmi Palestina kama taifa huru.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malta siku ya Jumatatu imetangaza kuwa nchi hiyo, wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, itaikubali rasmi Palestina.

Kwa hatua hii, Malta inajiunga na nchi nyingine ambazo katika siku za karibuni zimechukua msimamo kama huo. Jumapili iliyopita, Uingereza, Kanada, Australia na Ureno pia ziliitambua Palestina rasmi, ikiwa ni hatua iliyolenga kumaliza vita vinavyoendelea katika Ukanda wa Gaza.

Ni vyema kutambua kuwa Malta, kwa jina rasmi Jamhuri ya Malta, ni nchi ya kisiwa kilichopo kusini mwa Ulaya katikati ya Bahari ya Mediterania.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha